
Kitu kizuri ni kwamba Teknolojia imekuwa ikirahisisha vitu vingi sana sikuhizi… waliobuni hiki kifaa wamekipa jina la ‘Walk Car‘ yani wanakifananisha na gari linalomrahisishia mtu kutembea !!
Huu ni ubunifu wa jamaa toka Japan, kazi imefanywa na jamaa anayeitwa Kuniako Saito akishirikiana na wenzake wa Kampuni ya Cocoa Motors..
Uko ubunifu ulioitangulia hii, ni kile kifaa cha Hoverboard Segway au iohawk japo chenyewe kina changamoto zake.. kina matairi mawili tu, kama huwezi kutembea nacho unaanguka wakati wowote yani !!
WalkCar hiki hapa aisee, kifaa kidogo
kabisa kama laptop lakini kinaweza kukutembeza umbali wa Kilometa mpaka
10 kwa saa moja… uzuri mwingine ni kwamba Walk Car ina matairi manne na
kinatumia mfumo wa kuchaji kwa umeme.
Kifaa hiki Bei yake inagusa kama Dola 800 ambazo kwa Bongo inakuwa kama Tshs. Milioni 1.7 hivi !!
No comments:
Post a Comment